Waziri wa Mambo ya Nje wa
Cyprus. Dkt. Constantinos Kombos amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu
nchini na kuagwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam jana Julai 10, 2025.
Wakati wa ziara yake
nchini, Dkt. Constantinos Kombos alikutana na viongozi mbalimbali akiwemo
mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.
Balozi Mahmoud Thabit Kombo ambapo kwa pamoja walisaini Hati ya Makubaliano
Kuhusu Mashauriano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Cyprus ambayo yanatarajiwa
kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi baina ya mataifa hayo
mawili.
0 Maoni