Kamishna wa Uhifadhi,
Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Abdul-Razaq Badru ametembelea
maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa
sabasaba na kupongeza kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Akizungumza na waandishi
wa habari ndani ya banda hilo Kamishna
Badru amezipongeza taasisi hizo kwa kushinda tuzo nyingi zilizotolewa na
mtandao wa World Travel Awards (WTA) by 28 Juni, 2025.
Kamishna Badru
amewaeleza waandishi wa habari kuwa
sambamba na ushiriki wa Ngorongoro katika maonesho mbalimbali ili kujitangaza ,
pia mamlaka hiyo inaendelea kufanya jitihada za kuboresha miundombinu ya utalii
kama barabara, huduma za malipo, malazi kwa wageni na huduma za usafiri.
“Tumejipanga mwaka huu wa
fedha kuhakikisha kuwa barabara zetu zinaboreshwa na kupitika muda wote, kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali jitihada zinaendelea kuongeza miundombinu ya
malazi na huduma za usafiri ili kukidhi ongezeko la wageni wanaotembelea
vivutio vyetu kila mwaka,”alisema Kamishna Badru.
Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro inashiriki maonesho hayo ili kuendelea kutangaza vivutio vya utalii
kwa watembeleaji wa eneo hilo.
Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro mwaka huu 2025 limetangazwa na mtandao wa world Travel Awards ( WTA) kuwa kivutio bora cha utalii baranı Afrika ikiwa ni mara ya pili baada ya kushinda tuzo hiyo mwaka 2023.
Na. Hamis Dambaya - DSM
0 Maoni