Watumishi wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) Upanga na Mloganzila, leo Julai 27, 2025 wameshiriki mbio
za zilizoandaliwa na Benki ya Taifa ya Biashara, NBC Dodoma Marathon 2025 kwa
lengo la kuunga mkono juhudi za kuboresha huduma za afya, hususan afya ya mama
na mtoto pamoja na kuhamasisha umuhimu wa mazoezi kwa afya bora.
Akizungumza mara baada ya
kumaliza mbio hizo, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji MNH-Upanga Dkt. Rachel
Mhavile, amesema ushiriki wao ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za NBC katika
kuboresha huduma za afya nchini, hususan kwa mama na mtoto.
Dkt. Mhavile ameongeza
kuwa mazoezi ni muhimu kwa watumishi wa afya na jamii kwa ujumla, kwani
husaidia kuweka miili katika hali bora ya afya na kujikinga dhidi ya magonjwa
yasiyoambukiza.
0 Maoni