Kreta ya Ngorongoro
imetambuliwa na mtandao wa "Tripadvisor Travellers'" kuwa ni miongoni
mwa kivutio kinachoongoza na kupendwa na wageni (Top attraction) mwaka 2025,
ikishika nafasi ya sita katika vivutio bora barani Afrika.
Kreta ya Ngorongoro
imepewa hadhi na mtandao huo kuwa miongoni mwa asilimia 1 ya juu ya maeneo
yaliyotajwa na wageni duniani kote kwenye Tripadvisor ambapo tuzo hiyo hutolewa
kwa msingi wa maoni halisi ya watu waliotembelea na kutoa tathimini za kweli
kupitia mtandao wa Tripadvisor ndani ya kupundi cha miezi 12.
0 Maoni