Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa jana Julai 21, 2025 amewasili nchini Belarus kuanza ziara ya kikazi
nchini humo. Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kinsk alipokelewa na Naibu
Waziri Mkuu wa Beralus, Viktor Karankevich.
Katika ziara hiyo siku ya
Kwanza Mheshimiwa Waziri Mkuu ataweka shada la maua katika mnara wa mashujaa wa
Jamhuri ya Beralus.
Pia atatembelea kiwanda
cha kutengeneza Matrekta na vifaa mbalimbali
vya kilimo (Minsk Tractor Plant) na baadae atakutana na Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Belarus Mhe. Alexander Turchin.
Katika ziara hiyo
ameambatana na Balozi wa Tanzania Urusi
na Belarusi, Frederick Ibrahim Kibuta ,
Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais, Kazi , Uchumi na Uwekezaji Zanzibar,
Shariff Ali Shariff na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya
Mashariki, Cosato Chumi.
0 Maoni