Operesheni kubwa ya
uokoaji na utafutaji watu imeendelea usiku kucha huko Texas nchini Marekani baada
ya mafuriko ya ghafla kusababisha vifo vya watu wasiopungua 24 na kutoonekana
kwa wasichana wengi waliokuwa kwenye kambi
ya majira ya joto ya Kikristo.
Kulikuwa na onyo dogo
kabla ya Mto Guadalupe kujaa kwa futi 26 (sawa na mita 7.9) kwa muda wa chini
ya saa moja, na mafuriko yaliyofuata yalisomba nyumba kuhamishika, magari, na
vibanda vya mapumziko ambako watu walikuwa wakisherehekea wikendi ya tarehe 4
Julai.
Vikosi vya uokoaji
bado vinaendelea kuwatafuta hadi watoto 25 waliokuwa miongoni mwa wasichana 750
waliokuwa wakihudhuria Kambi ya Mystic, iliyoko nje kidogo ya mji wa Kerrville,
kilomita 104 kaskazini-magharibi mwa San Antonio.
Hali ya hatari
imetangazwa katika wilaya kadhaa ambapo barabara nyingi zimesombwa na maji na
mawasiliano ya simu yamekatika.
Rais wa Marekani
Donald Trump ameita tukio hilo "la kushtua" na "la
kutisha," huku ya Marekani White
House ikiahidi msaada wa ziada.
Picha zinaonyesha
maji mengi ya mafuriko yamejaa hadi juu ya madaraja na maji yanayotiririka kwa
kasi yakipita barabarani.
0 Maoni