Wambolezaji wawasili maziko ya Diogo Jota

 

Waombolezaji wameanza kuwasili kwa ajili ya mazishi ya mwanasoka Diogo Jota na mdogo wake André Silva katika mji wao wa nyumbani wa Gondomar, nchini Ureno.

Wanafamilia na viongozi wakuu kutoka dunia ya soka nchini Ureno wameonekana wakiwasili kwa ajili ya ibada hiyo ya mazishi mamia ya wananchi wamekusanyika nje ili kutoa heshima zao za mwisho.

Ndugu hao wawili walifariki katika ajali ya gari iliyotokea nchini Hispania siku ya Alhamisi maafisa wanasema gari lilitoka barabarani baada ya gurudumu kupasuka wakati walipokuwa wakijaribu kulipita gari jingine.

Mshambuliaji wa Liverpool, Jota, mwenye umri wa miaka 28, alifunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu, Rute Cardoso, siku 11 tu kabla ya ajali hiyo kutokea walikuwa na watoto watatu.



Chapisha Maoni

0 Maoni