Waziri Mkuu wa India,
Narendra Modi, ametembelea eneo la ajali ya ndege ya Air India iliyotokea
Alhamisi, ambapo watu wote isipokuwa mmoja kati ya 242 waliokuwa ndani ya ndege
hiyo waliaga dunia.
Ndege hiyo ilikuwa
ikielekea London kabla ya kuanguka kwenye eneo la makazi muda mfupi baada ya
kupaa.
Hadi sasa
haijafahamika ni watu wangapi waliopoteza maisha ardhini, ingawa afisa mmoja
ameiambia BBC kwamba watu wasiopungua wanane wamefariki dunia kutokana na ajali
hiyo.
Mtu pekee aliyeokoka
ni raia wa Uingereza, Vishwashkumar Ramesh, aliyekuwa ameketi kwenye kiti namba
11A, anaendelea kupata matibabu hospitalini. Kaka yake amesema "hatambui
namna alivyonusurika ajali."
Kwa mujibu wa shirika
la ndege la Air India, abiria waliokuwemo walijumuisha raia 169 wa India, 53 wa
Uingereza, saba wa Ureno na mmoja wa Canada.
Familia za
waliopoteza maisha zimeanza kutoa sampuli za vinasaba (DNA) kusaidia katika
utambuzi wa miili ya wapendwa wao.
0 Maoni