WAZIRI MKUU, Kassim
Majaliwa leo Juni 13, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye
kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa kuhusu Ualbino
yanayofanyika katika uwanja wa Mwanga Centre, mkoani Kigoma.
Kaulimbiu ya
Maadhimisho hayo kimataifa ni ‘Kudai Haki Zetu, Kulinda Ngozi Zetu, Hifadhi
Maisha Yetu’.
Aidha, Kitaifa,
kaulimbiu ya Maadhimisho hayo ni: “Ushiriki katika Uchaguzi ni Haki Yetu:
Kuchagua na Kuchaguliwa, Linda Haki za Watu Wenye Ualbino.”
0 Maoni