Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais - TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametoa rai kwa walimu nchini kuwa
wazalendo na kuzingatia weledi ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
Mhe. Mchengerwa
ametoa rai hiyo kwenye mkutano wa walimu na wadau wa elimu wa Wilaya ya Rufiji uliofanyika kwenye ukumbi
wa shule ya Sekondari ya Wasichana Bibi Titi Mohamed, ambapo yeye mwenyewe pia
alitunukiwa tuzo ya heshima ya kutambua mchango wake katika sekta ya elimu
wilayani Rufiji.
"Katika hali ya
kawaida Serikali imeboresha mazingira na
miundombinu ya sekta ya elimu kilichobaki ni kwa sisi walimu kutanguliza
uzalendo ili kuinua kiwango cha elimu katika ngazi zote," amesisitiza Mhe.
Mchengerwa.
Aidha, amesisitiza
walimu kutambua wajibu wao na kwamba Serikali haitaweza kusita kuwachukulia
hatua za kinidhamu Walimu na Maafisa
Elimu ambao watakuwa wazembe katika utekelezaji wa majukumu yao.
Katika taarifa ya
Wilaya ya Rufiji kwa Mhe. Waziri, iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Rufiji, bwana Simon Berege, inaonyesha
kuwa kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaohitimu darasa la Saba kutoka 3135 mwaka
2020 hadi wanafunzi 3715 mwaka 2024.
Idadi ya shule za
Awali na Msingi zimeongezeka kutoka 48
mwaka 2021 Hadi 63 mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la shule 15 sawa na asilimia
31.3.
Pia vyumba vya
madarasa vimeongezeka kutoka vyumba 377 mwaka2921 hadi vyumba566
mwaka 2025 ikiwa ni ongezeko la vyumba vya madarasa 189 sawa na asilimia 50. 1.
Aidha, katika
mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya mkoa, Halmashauri ya Mji wa Rufiji
imefanikiwa kushinda kwa nafasi ya kwanza katika michezo ya mpira wa miguu,
pete na riadha huku ikishika nafasi ya pili kwenye mpira wa mikono hivyo
kushika nafasi ya pili ya ujumla katika mashindano hayo.
Katika mkutano huo
Mhe.Waziri Mchengerwa alikabidhi makombe hayo kwa shule na baadaye kupokea
msaada wa madawati 50 yaliyotolewa na Benki ya CRDB.
Na. John Mapepele - Rufiji
0 Maoni