Serikali kupitia
bajeti yake ya mwaka 2025/2026 inakusudia kuzifanyia ukarabati shule zote
kongwe za msingi na sekondari zilizochakaa ili kuzirejesha katika mwonekano
wake wa awali.
Kauli hiyo imetolewa
leo Juni 04, 2025 bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI
(AFYA) Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge
katika kipindi cha maswali na majibu kwa
niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed
Mchengerwa.
Naibu Waziri Dkt.
Dugange amesema tayari OR – TAMISEMI imeianisha shule zote kongwe na chakavu
zinazohitaji ukarabati wa haraka na imefanya tathmini ya uhitaji wa fedha kwa
ajiri ya ukarabati wa shule hizo awamu kwa awamu.
Amesema katika bajeti
ya Serikali ijayo shule zote zilizo ainishwa zimepewa kipaumbele ambapo
zitakarabatiwa awamu kwa awamu kulingana na kiasi cha fedha kutoka Serikali Kuu
pamoja na upatikanaji wa fedha kupitia mapato ya
ndani ya Halmashauri.
Na. OR – TAMISEMI
0 Maoni