Watanzania 42
waliokwama nchini Israel kufuatia mapigano kati ya nchi hiyo na Iran, wanatarajiwa
kurejea nchini leo, Juni 25, 2025 kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la
Ethiopia (Ethiopian Airlines).
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa na Serikali, kurejea kwa Watanzania hao ni sehemu ya utekelezaji wa
maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia
Suluhu Hassan, aliyelitaka Serikali kuhakikisha wananchi wake waliokwama nje ya
nchi kutokana na hali ya machafuko, wanarejea nyumbani wakiwa salama.
Taarifa hiyo imeeleza
kuwa Watanzania hao watawasili nchini kwa makundi mawili. Kundi la kwanza
limewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Unguja
saa 6:55 mchana, huku kundi la pili likitarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam saa 11:55 jioni.
0 Maoni