Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika
pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika
Sala ya Eid Al Adha iliyosaliwa Masjid Taqwa, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar leo tarehe 7
Juni 2025.
Mapema baada ya sala
hiyo, Rais Dkt. Mwinyi alifika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja
kuchinja mnyama(Udh-hiya) ikiwa ni sehemu ya Ibada na kutoa mkono wa Eid
kwa Masheikh wa Mkoa huo.
0 Maoni