Waumini wa dini ya kiislam wilayani Rufiji wamefanya dua maalum ya kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na amani ya Tanzania kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa wananchi kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Baraza
la waislam Tanzania Wilaya ya Rufiji Shehe Ally Mbwana amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Idd leo
Juni, 7, 2025 waislam wa Rufiji wameamua kumwombea Mhe.Rais Samia na Tanzania
ili nchi iwe na amani na kuwa na mafanikio.
"Ndugu zangu leo
tunakwenda kuliombea taifa letu liendelee kuwa na amani pia kumwombea Mhe. Rais
wetu ili Mwenyezi Mungu amwezeshe aendelee kuliongoza vema taifa letu."
Amesema Shehe Mbwana.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais -TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ambaye pia ameshiriki kwenye dua
hiyo amefafanua kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na amani hivyo ni muhimu
kuilinda amani hiyo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.
" Watanzania
wenzangu,wa dini zote ni muhimu tukatambua maendeleo tuliyonayo sasa chini ya
uongozi thabiti wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan yanatokana na amani ambayo
imejengwa na viongozi wetu kuanzia enzi za baba wa taifa, mwalimu Nyerere hivyo
tusije tukathubutu kuichezea," amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Amesisitiza kuwa
amani inapovunjika familia hazikai pamoja, akina mama, watoto na wazee ndiyo
wanaoongoza kwa kuteseka hivyo ni muhimu kuilinda amani ya nchi yetu kwa kuwa
hatuna Tanzania nyingine.
Amemshukuru Mhe Rais kwa kutoa fedha kwa ajili y
a miradi mbalimbali ya elimu, afya na miundombinu
kwenye Halmashauri zote nchini ambapo amesema sekta hizo kwa sasa zimeboreshwa
kuliko awali katika kipindi kifupi cha Rais Samia.
Akitolea mifano ya
kuboreka kwa sekta hizo, Mhe. Mchengerwa
amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la vituo vya afya, shule za Msingi na
Sekondari katika jimbo la Rufiji.
Dua hiyo maalum ya
kumwombea taifa la Tanzania na Mhe. Rais na Serikali yake imefanyka kwenye
Msikiti wa Masjid Jumuiyya katika Mji wa Ikwiriri- Rufiji.
0 Maoni