Mamlaka ya
Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro imeanza utekelezaji wa mpango maalum wa
kuboresha eneo la Endoro ili litumike kama sehemu ya utalii tiba kwa
watalii pamoja na shughuli nyingine zinazohitaji utulivu.
Kamishna
wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Abdul-Razaq Badru
akiwa na Wakurugenzi wa Bodi katika eneo hilo lenye Maporomoko ya
Maji (Water Falls), Mapango ya Tembo, Msitu, Wanyama wakubwa na
maarufu kwa utalii wa kutembea (Walking Safaris).
Ameeleza kuwa
kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Utalii (TDL) eneo la Endoro
linaboreshwa kwa ujenzi wa miundombinu ya kisasa ya Utalii ili
yatumike kama sehemu za utalii tiba, utafiti, utalii wa kutembea,
mapumziko binafsi na kuondoa msongo wa mawazo.
“Endoro ni
eneo lenye utulivu, lina kivutio cha Mapango ya Tembo na maporomoko
ya maji yenye urefu wa mita 40, mamlaka imeamua kuboresha miundombinu
yake ili mgeni akifika hapa na hasira aweze kupata utulivu na kurudi
katika hali yake ya kawaida,” alisema kamishna Badru.
Makamu
Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt. Harieth Mtae amepongeza jitihada hizo na
kusema zitatoa fursa ya kuongezeka kwa idadi ya watalii
wanaotembelea kivutio hicho kilichopo hifadhi ya
Ngorongoro.
Wakurugenzi wa bodi hiyo pia wamekagua geti la
kisasa la kuingilia ndani ya hifadhi linalofanya kazi katika mfumo wa
kisasa pamoja na minara ya mawasiliano ndani ya hifadhi inayolenga
kuboresha huduma kwa watalii.



.jpeg)
0 Maoni