Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi kutoka Zanzibar wametembelea
hifadhi ya Ngorongoro na kustaajabishwa na historia ya binadamu,
malikale, Urithi wa Utamaduni na Wanyamapori na kutoa wito kwa watu
mbalimbali kutembelea hifadhi hiyo yenye hadhi tatu za Kimataifa
zinazotambuliwa na UNESCO
Akizungumza kwa niaba ya wabunge
hao mbunge wa viti maalum Mhe. Zainab Abdallah ameeleza kuwa katika
ziara hiyo wameshuhudia maendeleo yaliyotukuka kuhusu uhifadhi,
utalii, Malikale, urithi wa utamaduni na maendeleo ya jamii ambapo
vinadhihirisha kuwa Ngorongoro ni kivutio bora cha Utalii Barani
Afrika.
“Kuona ni kuamini, jana na leo tumetembelea eneo la
hifadhi ya Ngorongoro na tumeona maendeleo makubwa yakifanyika na kwa
macho yetu tumeshuhudia idadi kubwa ya watalii waliojawa na nyuso za
bashasha na furaha kwa kushuhudia vivutio vilivyopo, mandhari na hali
ya hewa ambayo unaipata Ngorongoro pekee”,amesema Mhe.
Zainab.
Wabunge katika ziara hiyo walielezwa kuhusiana na
historia ya kutokea kwa kreta ya Ngorongoro, chimboko la binadamu wa
kale na namna ambavyo mabadiliko ya viumbe mbalimbali yanavyoendelea
kutokea kwa nyakati tofauti.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Uhifadhi anayesimamia Idara ya maendeleo ya jamii, Gloria Bideberi
akizungumza kwa niaba ya kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro,
Abdul-Razaq Badru amewapongeza wabunge hao kwa kufanya maamuzi
sahihi ya kutembelea hifadhi hiyo yenye vivutio mbalimbali na
kuwaomba kuendelea kuwa mabalozi wa kuitangaza Ngorongoro ambayo
imepata tuzo ya kuwa chaguo la Wasafiri(Watalii) la kiwango cha Juu
cha Ubora mwaka 2026 (Travellers Choice Awards, Best of the best
2026)
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro linasifika duniani
kutokana na kuwa na ikolojia yenye mchanganyiko wa viumbe mbalimbali
kuishi kwa pamoja Ngorongoro kwa miaka mingi.


0 Maoni