Mbunge wa Jimbo la
Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amekabidhi jengo la kupumzikia wananchi
katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambalo litasaidia kutatua changamoto ya
wananchi wengi ambao hawakuwa na eneo lenye staha la kupumzika wakati wakiwa
wanawahudumia wagonjwa wao.
Hafla hiyo ya
kukabidhi jengo hilo imeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh. Rosemary S.
Senyamule leo tarehe 25.06.2025.
“Mh. Rais Dkt. Samia
S. Hassan amefanya kazi kubwa ya maboresho ya vifaa na huduma ya Afya kwenye
Hospitali hii ya Rufaa Dodoma.
Kazi iliyofanywa na
Mbunge Mavunde ni ya kuigwa mfano kwa kuwa ameunga mkono jitihada za Mh. Rais
kwenye maboresho ya huduma za Afya.
Jengo hili litasaidia
sana kuwafanya wananchi wa Dodoma na nje
ya Dodoma kukaa kwenye mazingira mazuri na nadhifu,hivyo naagiza jengo hili
kutunzwa na kusimamiwa vyema kwa lengo lililokusudiwa.
Nakupongeza pia
Mbunge Mavunde kwa kuanzisha ujenzi wa uzio wa Hospital ya Rufaa,nitoe rai kwa
wadau wengine kuunga mkono jitihada hizi kubwa za Mbunge katika kuweka uzio wa
Hospitali ya Rufaa,” alisema Senyamule.
Akitoa taarifa ya
awali,Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dkt. Ernest Ibenzi amesema
Hospitali hiyo hivi sasa inaendelea na upanuzi mkubwa na ujenzi wa majengo
mapya ya kutoa huduma kwa wananchi na hivyo kutumia nafasi hiyo kumshukuru
Mbunge Mavunde kwa ushirikiano mkubwa ambao amekuwa akiutoa kwenye Hospitali
ikiwemo ya ujenzi wa jengo la wananchk na hatua ya kuanzisha ujenzi wa uzio wa
Hospitali hiyo.
Akizungumza katika
hafla hiyo Mbunge Anthony Mavunde amesema ujenzi wa jengo hilo umechochewa na
idadi kubwa ya wananchi ambao wanafika Hospitalini hapo kwa ajili ya
kuwahudumia wagonjwa wao na kukosa maeneo ya kupumzika hasa nyakati za usiku.
Sambamba na ujenzi wa
jengo hilo,pia ameahidi kukamilisha ujenzi wa uzio wa eneo la mbele la
Hospitali ya Rufaa Mkoani Dodoma.




0 Maoni