Balozi wa China Nchini, Chen Mingjian ametembelea Hifadhi ya Urithi wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songomnara jana Juni 24,2025.
Katika safari yake
alipata kujionea vivutio vya utalii vilivyopo katika Magofu ya Kilwa Kisiwani
na kupata maelezo kuhusu historia ya Biashara kati ya Kilwa Kisiwani na China
mnamo karne ya 13 kutoka kwa wahifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori
Tanzania.
Balozi Chen Mingjian
aliambatana na watalii wengine 10 kutoka Nchini China pamoja na Mkuu wa Wilaya
ya Kilwa, Mhe.Mohamed Nyundo.
0 Maoni