Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wanajamii kujiepusha na mazingira yanayoweza kusababisha migogoro baada ya wao kufariki
Dkt.
Biteko amesema hayo Mei 23, 2025 Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua
Kongamano na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wanasheria Wanawake nchini -
TAWLA
Amesema
endapo wanajamii watajiandaa na kuweka mazingira mazuri, wataepusha migogoro
isiyo ya lazima na jamii itaishi kwa amani na kupunguza gharama zinazotumika
kurekebisha jamii yenye migogoro
Aidha,
ameipongeza TAWLA kwa kazi nzuri iliyodumu kwa miaka 35 tangu kuazishwa kwake
mwaka 1990
“
Tangu mlipoanzishwa kuna vyama vingi vya kijamii vilianzishwa sambamba na chama
chenu, lakini vingine vilikufa baada ya mwaka mmoja, vingine vilikufa baada ya
miaka mitano na vingine vilisambaratika baada ya miaka 10. Ninyi mmeimarika na
kukua hadi leo na mnaendelea kufanya kazi nzuri,” ameoongeza Dkt. Biteko
Pia
amewasilisha pongezi za Rais Samia kwa TAWLA kupitia kushiriki kampeni ya
msaada wa kisheria ya Samia Legal Aid na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea
kushirikiana nao kuhakikisha jamii inaishi kwa amani na upendo kama ilivyo
ndoto ya TAWLA ya kuwasaidia watu wenye uhitaji.
“Bila
mchango wenu, mafanikio yanayozungumzwa serikalini huenda yasingekuwa
yanazungumzwa kwa kiwango hicho, amesema Dkt. Biteko
Ameutaka
uongozi wa TAWLA kuendelea kuwashawishi na kuwavutia wanachama wapya
watakaoweza kutoa msaada bila kusita katika jamii yao.
Amesema
Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuhakikisha wanawake wanakuwa katika
nafasi mbalimbali za maamuzi ikiwemo kuongeza uwiano wa majaji wanawake na
wanaume katika mahakama za rafani na mahakama Kuu Akizungumzia Uchaguzi Mkuu
ujao, Dkt. Biteko amewahimiza wajumbe wenye nia kujitokeza na kugombea uongozi
ili kuwakilisha wananchi hususan wanawake wanaongezeka
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila ameipongeza TAWLA
kwa kazi ya kutetea kundi maalum la wanawake na kuliwezesha kupata msaada wa
kisheria
“TAWLA
inafanya kazi kubwa ya kufanyia kazi tabia za watu na kazi hiyo inahitaji
mawanda mapana” amesema na kuongeza kuwa wadau wa sheria wanashughulia watu
wenye malezi na makuzi tofauti hivyo, kazi yao ni kubwa inayohitaji kufanyika
kwa weledi wa hali ya juu.
Mwenyekiti
wa TAWLA Wakili Suzan Ndomba ameipongeza Serikali kwa hatua zake za kulinda
haki na kushughulikia changamoto za zinazowakabili wanawake na watoto nchini
Amesema
hatua ya Serikali kuwekeza katika utekelezaji wa miradi ya nishati, maji na
elimu ni fursa zaidi kwa kundi la wanawake wa Tanzania ambao wamekuwa
waathirika wakubwa madhara yanayotokana na ukosefu wa miundombinu hiyo
Amefafanua
kuwa tangu kuanzishwa kwa TAWLA, chama hicho kimeshiriki kutoa mafunzo kwa
baadhi ya mawakili, kuanzisha huduma ya simu ya bure kwa ajili ya wateja wake
kurupoti vitendo na matukio ya ukatili, kuwatetea wateja wake mahakamani,
kushiriki katika kuandaliwa na kutungwa kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009
pamoja na kutungwa kwa kifungu maalum cha makosa ya kujamiiana SOSPA (2008).
TAWLA
ilianzishwa mwaka 1990 ikiwa na wanachama 40 na idadi yao imeongezeka hadi 420
miaka 35 baadaye.
0 Maoni