Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Maafisa Habari Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Seriksali za Mitaa kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Waziri
Mchengerwa ametoa wito huo leo, wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa Habari
wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi za Ofisi ya Rais-TAMISEMI
kinachofanyika katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma uliopo kwenye Mji wa Serikali
Mtumba mkoani Dodoma.
“Mmebeba
dhamana kubwa ya kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi hivyo msiwaache
watanzania walishwe habari potofu” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.
Mhe.
Mchengerwa amesema kuwa, Maafisa Habari nchini ni rasilimaliwatu muhimu hivyo
wakitambua wajibu wao na kujiimarisha kiutendaji ni wazi kuwa wananchi watapata
taarifa sahihi kwa wakati.
“Iwapo
kila mmoja wenu akiwa mzalendo na kutambua wajibu wake, habari mtakazozitoa
ndio zitaaminiwa na kupokelewa na watanzania kupitia vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii ambayo imeshamiri hivisasa,” Waziri Mchengerwa amehimiza.
Waziri
mchengerwa amesema, ana amini kwamba maafisa habari waliopo wana weledi na
ujuzi unaowawezesha kutoa taarifa sahihi zenye tija kwa wananchi na maendeleo
ya taifa kwa ujumla.
Sanjari
na hilo, Waziri Mchengerwa ameelekeza Maafisa Habari wa Mikoa na Mamlaka za
Serikali za Mitaa washiriki kwenye ziara za viongozi ili wapate uelewa
utakaowawezesha kutangaza kwa ufanisi mafanikio ya Serikali katika utekelezaji
wa miradi ya maendeleo.
Aidha, Waziri Mchengerwa amewaelekeza waajiri katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha Maafisa Habari wanaokaimu ukuu wa vitengo ambao wana sifa, wapewe vitengo ili waweze kutekeleza kikamilifu jukumu la kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi zao ikiwa ni pamoja na kutangaza mafanikio yaliyopatikana kwenye eneo la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambalo limepewa kipaumbele na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Na.
James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
0 Maoni