Utawala wa Rais Donald Trump siku ya Alhamisi umeondao uwezo wa Chuo Kikuu cha Harvard kuandikisha wanafunzi wa kimataifa, na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya taasisi hiyo ya kifahari iwapo itataa kutii matakwa ya sera za utawala huo.
"Harvard haiwezi tena kuandikisha wanafunzi
wa kigeni na wanafunzi wa kigeni waliopo lazima wahamie vyuo vingine au
wapoteze hadhi yao ya kisheria," ilisema taarifa ya Idara ya Usalama wa
Ndani ya Marekani.
Hatua hii ya kushangaza imekuja wakati wanafunzi
kutoka kote duniani walikuwa wakijiandaa kuhudhuria Harvard, chuo kikuu cha
zamani zaidi Marekani na mojawapo ya taasisi zinazoheshimiwa sana nchini humo
na kimataifa.
Uamuzi huu utawaaathiri zaidi ya robo ya idadi ya wanafunzi wa Harvard, wengi wao wakiwa ni wa kimataifa, ambao sasa wamejikuta kwenye hali ya wasiwasi na mkanganyiko kutokana na tangazo hilo.
0 Maoni