Waziri Mkuu wa
Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameondoka jana nchini kwenda Japan
kumwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maonesho ya World
Expo 2025 Osaka.
Taarifa iliyotolewa
na Ofisi ya Waziri Mkuu imesema pamoja na mambo mengine Mhe. Majaliwa
atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahususha
wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.
Pia, Waziri Mkuu
atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati
ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo
yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajiwa kumalizika Oktoba 13, 2025. Hii
ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho hayo ya kimataifa
ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).
0 Maoni