Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amezindua
rasmi leo hii maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani na kuwasihi wadau wa sekta
ya nyuki na misitu pamoja na utalii kutembelea mabanda yaliyoko katika maonesho
ili kupata elimu na maarifa kutoka kwa wadau wa sekta ya Maliasili na Utalii
kuhusu shughuli za Ufugaji wa Nyuki.
Maadhimisho hayo yaliyozinduliwa leo hii yanafanyika katika
viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma kuanzia Mei 17 hadi 20, 2025
yakiongozwa na kauli mbiu isemayo "Nyuki kwa Uhai na Uchumi Imara,
Tuwahifadhi" Apimondia 2027 Tanzania Ipo Tayari.
Mhe. Senyamule amesema kauli mbiu hii inawakumbusha
Watanzania kuhusu mchango wa Nyuk katika afya zetu kutokaka na matumizi ya
mazao mengi anayozalisha kama vile chavua, sumu pamoja na maziwa ikiwa ni
pamoja na kujipatia kipato kupitia mazao hayo.
Aidha amefurahishwa na biadhaa mbalimbali zilizotenengezwa
na wafanyabiashara na wajasiriamali ikiwamo zile zitokanazo na mazao ya nyuki
wakati akifanya ziara yake katika mabanda ya maonesho akisema ni kielelezo kuwa
bidhaa zitokanazo na Nyuki ni tiba kwa matumizi mballimbli ya afya lakini pia
ni sehemu ya kupata kipato na kujiiunua kiuchumi.
“Nimeona watu wakiuza asali ambapo watu wanapata kipato na
wakuwa kiuchumi, nimeona watu wakitengeneza mazao mbali mbali ya Nyuki,”
alisema.
Pamoja na hayo amesema kuwa maonesho haya yatafungwa rasmi na Mhe. Kassima Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kama mgeni rasmi huku akitoa wito kwa wananchi wote wa mkoa wa Dodoma kuungana na Waziri Mkuu katika kufunga maonesho hayo.
0 Maoni