Rais wa zamani wa Marekani, Joe Biden, mwenye umri wa miaka
82, amegundulika kuwa na Saratani ya tezi dume ambayo imeenea hadi kwenye
mifupa, kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi yake iliyotolewa Jumapili.
Biden, ambaye aliondoka madarakani mwezi Januari 2025,
aligundulika na ugonjwa huo siku ya Ijumaa baada ya kwenda kumuona daktari wiki
iliyopita kutokana na dalili za kwenye mkojo.
Saratani hiyo ni aina kali zaidi ya ugonjwa huo, ikielezewa
kuwa na alama ya Gleason ya 9 kati ya 10. Hii ina maana kuwa ugonjwa wake
umeainishwa kama wa "daraja la juu," na seli za saratani zinaweza
kusambaa kwa haraka, kulingana na shirika la Cancer Research UK.
Biden na familia yake wameripotiwa kuwa wanapitia chaguzi mbalimbali za matibabu. Ofisi yake iliongeza kuwa saratani hiyo ina uhusiano na homoni, jambo linalomaanisha kuwa ina uwezekano mkubwa wa kudhibitiwa.

0 Maoni