Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan ametangaza kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma
kwa asilimia 35.1, ambayo nyongeza hiyo itaanza kutumika mwezi wa Julai 2025.
Dkt. Samia ametangaza nyongeza hiyo leo kwenye Maadhimisho
ya Siku wa Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo Kitaifa Sherehe hizo zimefanyika
katika uwanja wa Bombadia Mkoani Singida tarehe 01 Mei, 2025.
"Ninayo furaha ya kuwatangazia kwamba katika kuzidi kuleta ustawi kwa wafanyakazi, mwaka huu, Serikali itaongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1, nyongeza hiyo itaanza kutumika mwezi wa Julai 2025," alisema Dkt. Samia.
Nyongeza hiyo itafanya sasa mshahara wa kima cha chini kutoka shilingi 370,000 hadi shilingi 500,000, ambapo ngazi nyingene za mshahara nazo zitapanda kwa viwango tofauti tofauti kulingana na uwezo wa kibajeti.
0 Maoni