Makumi ya viongozi mashuhuri wakiwamo Marais Donald Trump, Volodymyr Zelensky, pamoja na Prince William wanashiriki misa ya mazishi ya Papa Francis.
Viongozi hao wameungana na waombolezaji wapatao 200,000
wakiwemo 50,000 ndani ya Kanisa la Mtakatifu Peter's Square kushiriki misa hiyo.
Rais Trump na Zelensky walikutana kabla ya shughuli ya mazishi,
huku Ikulu ya Marekani ikisema mkutano wao ulikuwa wenye manufaa.
Rais Trump yupo mstari wa mbele katika misa hiyo pamoja na marais wa Finland na Estonia, ambao ni vinara wanaoiunga mkono Ukraine.
0 Maoni