Serikali imetoa zaidi ya Bilioni 37 kuboresha DIT Mwanza

 

Katika kuendelea kuboresha sekta ya elimu serikali imetoa zaidi ya bilioni 37 kwa ajili ya kuboresha taasisi ya Dar es Salaam Kampasi ya Mwanza DIT ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi wa kutengeneza bidhaa za ngozi na kuweza kujiajiri.

Serikali imeamua kuboresha majengo, ununuzi wa vifaa vya kisasa pamoja na kuhakikisha walimu wanapata ujuzi kutoka vyuo mbalimbali nchini vya ngozi ajili ya kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaotakiwa ili wanapojiajiri bidhaa zao ziendane na soko la sasa.

Mkurugenzi wa elimu ufundi kutoka Wizara ya Eimu na Sayansi ambaye pia ni mratibu wa mradi wa ESTRIP Dk. Fredrick Selukele amesema lengo la serikali kuweka mazingira wezeshi kwenye taasisi za ufundi ni kuhakikisha wanaongeza masoko ya nje ya uuzwaji wa bidhaa za ngozi.

“Nimesema huu ni mradi wa kikanda kwahiyo kuna wenzetu wa Ethiopia pia ni wafugaji kwahiyo ni fursa kwa wenzetu kubadilishana uzoefu na kubadilishana wanafunzi na ujuzi kwenye kuichakata ngozi kuweza kuingiza bidhaa zinazoweza kuingia soskoni na kutumika,” alisema Dk. Selukele.

Kwa upande wale mkuu wa taasisi ya Dar es Salaam DIT Preksedis Ndomba ameishukuru serikali kutoa fedha hizo kwa ajili ya kuboresha taasisi hiyo hali itakayosaidia kutekeleza vizuri sera mpya ya elimu na mafunzo yam waka 2014 toleo jipya la mwaka 2023.

“Sera mpya ya elimu toleo jipya la 2023 linasisitiza ujuzi na ujuzi huu tusingeweza kufika popote bila huu msaada DIT tuna dhana yetu inaitwa mafunzo viwandani kama shamba darasa kwahiyo kwa teknolojia na uhandisi tukasema kiwanda kiwe ndiyo darasa kwa serikali imetusaidia na kutuwezesha kutekeleza vizuri hiyo sera, na kama utaona utakutana na sehemu kubwa kabisa ya mradi huu ni kiwanda kile cha ngozi unachakata ngozi, lengo kuchachua sekta ya ngozi na kulipa thamani zao la ngozi,” amesema Ndomba.




Chapisha Maoni

0 Maoni