Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEM Mhe. Zainab Katimba
amesema Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya afya kwa kutenga bajeti
kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa, vifaa tiba na kuajiri watumishi wa
kada mbalimbali za afya kwa ajili ya hospitali za Wilaya nchini ikiwemo
Hospitali ya Mabogini.
Mhe. Katimba ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma katika
kipindi cha Maswali na Majibu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalumu
Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Zuena Athuman Bushiri aliyeuliza.
“Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka gari la wagonjwa,
vifaa tiba na wataalam katika Hospitali ya Wilaya ya Mabogini, Moshi Vijijini?.”
“Serikali katika mwaka wa fedha 2021/22 ilinunua magari 594
(ambulance 382 na, usimamizi 212) ya kubebea wagonjwa na usimamizi wa huduma za
afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
imepokea magari 2 ya kubebea wagonjwa na kupelekwa Kituo cha afya cha Umbwe na
Himo,” amesisitiza
Amesema Hospitali ya Wilaya ya Mabogini katika mwaka wa
fedha 2024/25 imepelekewa shilingi milioni 165 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa
tiba. Aidha, vifaa tiba vimeshanunuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya
Mabogini.
Hospitali ya Mabogini inajumla ya watumishi saba (7) wanaotoa huduma katika hospitali hiyo kwa sasa.
Na. OR-TAMISEMI

0 Maoni