Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa waumini wa Kanisa Katoliki duniani, kufuatia kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis aliyefariki dunia leo Jumatatu ya Pasaka Aprili 21, 2025 akiwa na umri wa miaka 88.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Rais Dkt. Samia ameandika:-
Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa
Katoliki Duniani, Papa Francisko. Katika kipindi chote cha miaka 12 akiwa
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko ameishi maisha yake kama
mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo ya watu
pamoja na kudumisha amani.
Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa
nchini na duniani kote.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi.
Amina.

0 Maoni