Papa Francis afariki dunia

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis amefariki dunia leo Aprili 21,2025 akiwa na umri wa miaka 88, taarifa ya Vatican imesema.

Idara ya Habari ya Vatican, imesema Papa Francis amefariki dunia akiwa kwenye makazi yake ya Vatican, ya Casa Santa Marta.

“Katika maisha yake yote Papa Francis alijitolea kumtumikia Mungu na Kanisa lake,”Kardinali Kevin Farrell  amesema.

Kifo chake kimetokea siku moja tu baada ya kuonekana Kanisa la St Peter's Square kuwatakia Pasaka Njema maelfu ya waombaji.




Chapisha Maoni

0 Maoni