Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt.
Emmanuel John Nchimbi, ametoa salamu za Sikukuu ya Pasaka katika Tamasha la
Mtoko wa Pasaka lililoandaliwa na Wasanii wa Muziki wa Injili nchini.
Hafla hiyo iliyofanyika Jumapili tarehe 20 Aprili 2025
katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam, ilihusisha wasanii
nguli wa muziki huo, wakiongozwa na Christina Shusho, kupitia taasisi yake ya
Relax East Africa Limited.
Akizungumza katika tukio hilo, Dkt. Nchimbi alisisitiza
umuhimu wa kudumisha mshikamano, amani, na upendo miongoni mwa Watanzania.
Alihimiza jamii kuendeleza maadili mema na kuimarisha mshikamano wa kitaifa
kama msingi wa maendeleo endelevu.







0 Maoni