Rais Samia ampongeza Simbu kwa ushindi Boston Marathon

 

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza mwanariadha Mtanzania Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya pili katika Mashindano ya Kimataifa ya Mbio ya Boston (Boston Marathon).

Kupitia akaunti zake za mitandao ya jamii Rais Dkt. Samia ameandika yafuatayo:-

Pongezi za dhati kwa Alphonce Simbu kwa kushika nafasi ya pili katika Mashindano ya Kimataifa ya Mbio ya Boston (Boston Marathon). Umefanya kazi nzuri.

Ushindi wako ni matokeo ya kujituma kwa bidii, maandalizi mazuri, nidhamu yako kuanzia jeshini, kwenye mazoezi hadi kwenye mashindano, ukilibeba kwa heshima ya hali ya juu jina la nchi yetu.

Endelea kuipeperusha vyema bendera ya Taifa letu.

Chapisha Maoni

0 Maoni