Mwenyekiti wa Bodi ya Mwananchi Communications Limited (MCL), David Nchimbi amemtangaza Rosalynn Mndolwa-Mworia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MCL kuanzia leo.
Rosalynn anachukua nafasi hiyo, akimrithi Bakari Machumu aliyestaafu kwa hiari tangu Agosti mwaka 2024 na wadhifa huo kukaimiwa na Victor Mushi kwa miezi minane.
Nchimbi ametoa taarifa ya kupatikana kwa Mkurugenzi Mtendaji huyo mpya leo, Jumanne Aprili 29, 2025 katika kikao kilichohusisha Bodi ya Nation Media Group (NMG) na wafanyakazi wa MCL.
Wakati Rosalynn akichukua nafasi hiyo, Mushi ameteuliwa
kuongoza Idara ya Ubunifu NMG.
0 Maoni