Mahitaji ya juu ya umeme katika Gridi ya Taifa yameongezeka na kufikia MW 1,921.44 zilizofikiwa tarehe 09 Aprili, 2025 saa 3:00 usiku ikilinganishwa na MW 1,590.10 zilizofikiwa tarehe 26 Machi, 2024 saa 3:00 usiku sawa na ongezeko la asilimia 20.84.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwasilisha Hotuba ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa mwaka 2025/2026 leo Aprili 28, 2025 bungeni jijini Dodoma.
Aidha, amesema tangu mwaka 2020 kumekuwepo na ongezeko kubwa la mahitaji ya umeme nchini la MW 740.91 kutoka MW 1,180.53 za mwaka 2020 hadi MW 1,921.44 zilizofikiwa tarehe 09 Aprili, 2025, kutokana na ukuaji wa uchumi na kuimarika kwa utoaji wa huduma ya umeme kwa wananchi.
0 Maoni