Mbunge wa
Jimbo la Ilala kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Azzan Zungu,
amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya
kupata kura 378 kati ya kura 380 zilizopigwa na wabunge.
Uchaguzi huo
umefanyika leo, Novemba 11, 2025, katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma, ambapo
Zungu amewashinda wagombea wengine watano waliokuwa wakigombea nafasi hiyo
kupitia vyama vya NRA, DP, ADC, NLD, na AAFP.
Zungu,
ambaye alikuwa Naibu Spika wa Bunge katika Bunge lililopita, sasa anakuwa rasmi
kiongozi wa mhimili huo wa dola, katika Bunge la 13 lililoanza rasmi leo jijini
Dodoma.
Aliyekuwa
Spika wa Bunge lililomalizika, Dkt. Tulia Ackson, alijitoa katika mbio za
kuwania tena nafasi hiyo siku chache zilizopita bila kueleza sababu za uamuzi
wake huo.

0 Maoni