Kufuatia matukio ya hivi karibuni ya uchafuzi wa amani na uharibifu wa mali huko Arusha, Watanzania wameungana na kutoa wito wa kitaifa wa kurejea kwenye hekima, upendo na umoja, huku wakikataa vikali vitendo vya vurugu.
Ingawa vituo vya mafuta viliungua, ofisi
ziliharibiwa, na biashara kusimama kwa muda, jiji la Arusha sasa limesimama
tena, likisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo.
Akizungumzia hali ya mji huo, Josephat Akiiro,
alisema kuwa Arusha imeonyesha ukomavu baada ya changamoto:
"Vituo vya mafuta vimeungua. Ofisi zimeharibiwa.
Biashara zimesimama. Lakini leo, Arusha imesimama tena, kama jiji la hekima,
umoja, na matumaini."
Akiunga mkono kauli hiyo, Mwananchi wa Arusha mjini,
Hanifa alisisitiza kuwa vurugu haina nafasi:
"Vurugu haina faida, bali amani ndiyo msingi wa
maendeleo na heshima ya taifa. Tuchague amani, tujenge tena. Kwa Arusha. Kwa
Tanzania."
"Watanzania, Upendo Ndio Dira Yetu! Tujenge
Daraja la Upendo linalounganisha kabila, dini, na itikadi zetu... Tupendane,
tuheshimiane, na tushirikiane kwa moyo mmoja ili Tanzania iendelee kung'ara.
Amani yetu ni urithi wetu, tuulinde kwa Upendo!" alisema
Kwa upande wake, Bi. Latifa Merinyo alisisitiza kuwa
wanapaswa kuepuka upotoshaji,tulinde tunu ya amani kwa maendeleo ya nchi.
Bi Latifa alisema hayo huku akikariri, maneno ya
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alisema:"Ukiona mtu
anataka kuharibu amani ujue anaujihumu uhuru wetu. Tusikubali kutumiwa kuvuruga
tulichokijenga kwa miaka mingi."
Wananchi wengi waliohojiwa wamehimiza kuendelea
kulinda amani na mali za umma, wakisisitiza kwamba "Uchafuzi wa Amani sio
Desturi za Mtanzania" na kwamba "Amani Yetu, Fahari Yetu."

0 Maoni