Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu ametangaza
Jina la Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya
kupokea ujumbe maalum kutoka kwa Mpambe wa Rais (ADC) Brigedia Jenerali
Nyamburi Mashauri kuhusu uteuzi huo Bungeni leo Novemba 13, 2025.
Rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt.
Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jina la
Mbunge huyo wa Iramba Magharibi, ambaye alikuwa Waziri wa Fedha, limewasilishwa
Bungeni kwa ajili ya Waheshimiwa Wabunge kumthibitisha kuwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

0 Maoni