Wizara ya Maliasili na utalii, kupitia shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA) imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 41.13 katika eneo la
Kunzugu, Kata ya Balili, Mjini Bunda kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za TANAPA
Kanda ya Magharibi.
Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alipokuwa akijibu swali la Mhe. Robert Chacha Maboto
aliyetaka kujua Serikali itajenga lini Makao Makuu ya TANAPA katika Halmashauri
ya Mji wa Bunda.
Aidha, Mhe. Kitandula aliongeza kuwa Serikali imekamilisha
zoezi la upembuzi yakinifu na uandaaji wa michoro kwa ajili ya ujenzi wa ofisi
hiyo. Kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza kwenye mwaka wa fedha 2025/2026.
0 Maoni