Mkurugenzi wa Idara ya Afya Lishe na Ustawi wa Jamii, Ofisi
ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume
ameuelekeza uongozi wa kituo cha afya cha Buguruni kudhibiti mianya ya
upotevu wa fedha katika kituo hicho ili kuendelea kuboresha miundombinu ya
kituo na kufanikisha utoaji wa huduma kwa wananchi .
Dkt. Mfaume ametoa maelekezo hayo mara baada ya kutembelea
na kukagua upatikanaji wa huduma za Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii katika kituo
cha afya cha Mnazi Mmoja na kituo cha afya cha Buguruni.
“Tunapolenga upatikanaji wa huduma za afya kwa ubora zaidi
lazima tudhibiti mianya ya upotevu wa fedha na kuongeza mapato kwa kutoa huduma
bora Kwa wateja wetu,” amesisitiza Dkt. Mfaume.
Aidha, Dkt. Mfaume ametaka timu ya Usimamizi wa Huduma za
Afya (CHMT) katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuongeza usimamizi wa
fedha katika kituo vituo mbalimbali katika Halmashauri hiyo.
Pia Dkt. Mfaume ameielekeza timu ya Usimamizi wa Huduma za
Afya (CHMT) kushirikishana na Viongozi wa Serikali za Mitaa ili kufanikisha
utoaji wa huduma chanjo Kwa Watoto katika Halmashauri hiyo.
0 Maoni