Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia
Mradi wa Uboreshaji wa Barabara Vijijini kwa Ushirikishaji wa Jamii na
Ufunguaji wa Fursa za Kijamii na Kiuchumi (RISE) imefungua zoezi la kuweka wazi
jedwali la fidia kwa wananchi watakaoathiriwa na mradi wa ujenzi wa barabara ya
Sindeni - Kwedukwazu yenye urefu wa 38km inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha
lami katika kata ya Sindeni, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Zoezi hilo linaratibiwa na kusimamiwa na wataalamu wa TARURA
wakishirikiana na Mhandisi Mshauri anaye
"design" barabara hiyo ambapo lengo la zoezi hilo ni kuwapatia
wananchi viwango vya fidia kwa maeneo yatakayopitiwa na Mradi baada ya maeneo
yao kufanyiwa tathmini.
Barabara hiyo inatarajiwa kufungua na kuchochea shughuli za kiuchumi na kijamii pamoja na kuunganisha vijiji vya Kweisasu, Mbuyuni, Kwankono, Komfungo, Komdudu, Sindeni na Sezakofi katika kata ya Sindeni, wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.
0 Maoni