Balozi Nchimbi aanza ziara yake mkoani Mara

 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amezungumza na wananchi wa Bunda mkoani Mara alipowasili eneo hilo kwa kusalimiana nao, akiwa safarini kuelekea Musoma.

Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa mikutano yake na wananchi na wanachama wa CCM, ambapo Balozi Nchimbi anatarajiwa kutembelea wilaya mbalimbali katika Mkoa wa Mara kwa kipindi cha siku tano.

Katika salamu zake kwa wakazi wa Bunda, Dkt. Nchimbi amesisitiza dhamira ya CCM kuendelea kusikiliza wananchi na kuhakikisha maendeleo yanawafikia kwa wakati.

Ziara hiyo inatarajiwa kuhusisha mikutano ya hadhara, vikao na viongozi wa chama na serikali, pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo katika maeneo husika.



Chapisha Maoni

0 Maoni