Mamlaka
ya Hifadhi ya Ngorongoro imekutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii
duniani katika maonesho ya Magical 2025
yanayoendelea nchini Kenya wengi wakivitiwa na habari za vivutio vya utalii
vilivyoko Ngorongoro na kuinyesha dhamira ya kutembelea hifadhi hiyo.
Afisa
Utalii na Masoko Mkuu wa Mamlaka hiyo Michael Makombe amewaeleza wadau hao kuwa
hifadhi ya Ngorongoro imeendelea kuwa kivutio bora cha utalii baranı Afrika
kutokana na weledi wake wa kusimamia uhifadhi,utalii na maendeleo ya jamii.
“Tumefarijika
kuona katika maonesho haya wageni ambao hawajafika Ngorongoro wametamani
kufika,lakini tumewatembelea katika mabanda yao na kuwaeleza vivutio vyetu tulivyo
navyo na wengi wameonesha nia ya kufika Ngorongoro,” alisema Makombe.
Maonesho
hayo yanahusisha wadau wa sekta ya utalii kutoka mataifa mbalimbali duniani
ambapo pamoja na kuonesha shughuli zao wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu
katika sekta hiyo.
Na. Hamis
Dambaya - Nairobi Kenya
0 Maoni