Imeelezwa
kuwa wazee wanaume wanapofikia umri wa kustaafu wanakuwa wazito sana kutoka na
kushirikiana na jamii, jambo ambalo linaathari kutokana na takwimu kuonesha
wazee wanaume wanakufa haraka kuliko wazee wanawake kwa sababu wanapenda kujifungia.
Hayo
yameelezwa na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Philemon Foundation, Bw. Rodgers Mbaga katika Maadhimisho ya Siku
ya Wazee Duniani Oktoba mosi, ambapo amewashauri wazee wanaume kuachana na
tabia hiyo.
“Hili la
wanaume wazee kutopenda kutoka na kujumuika na jamii limejitokeza hata leo sisi
tumewaalika wazee wapatao 200, lakini cha kushangaza wengi wa wazee waliotoa
udhuru wa kutoshiriki kwa sababu mbalimbali ni wanaume,” alisema Bw. Mbaga.
Bw. Mbaga
amewapa changamoto wanaume kujenga utayari wa kutoka na kuchangamana na jamii
kwani kufanya hivyo ndio nafasi pekee ya kukabilian na misongo ya mawazo inayotokana
na changamoto za maisha.
“Wanaume
wengi pengine wakitoka sana wanaenda baa kupata kinywaji pengine wanadhani
inawasaidia kupoteza mawazo, lakini wanakosa fusa nyingine zaidi ya kukutana na
wazee wenzake na kubadilishana mawazo,” alisema Bw. Mbaga.
Bw. Mbaga
ameeleza kwamba taasisi ya Philemon Foundation imekuwa ikijishughulisha na
kundi la wazee wenye kipato cha kati, kutokana na kuwa Serikali mara nyingi
imekuwa ikijishughulisha na kundi la wazee masikini.
“Lakini
kuna kundi la wazee ambao suala la kujimudu kimaisha haliwapi shida sana, lakini
wanashida ya upweke, wamesahaulika kwa sababu kila mtu kwenye jamii anamini
hawa wapo kwenye maisha ya kujiweza hivyo hawana shida,” alisema Bw. Mbaga.
Amelitaja
kundi hiyo ambalo jamii imelisahau kuwa ni la wazee wastaafu wa taasisi
mbalimbali za umma na binafsi, wazee wastaafu wa shughuli zao binafsi zikiwamo za
wafanyabishara na wakulima.
“Wazee
hawa wengi wanaishia nyumbani wanachanganyikiwa hawatoki kwenda kazini, kwenda
kwengine kwa hiyo wanakosa kuwa sehemu ya jamii, wengi watoto wao wamesha
jiweza wanajitega wanakuwa wapweke,” alisema Mbaga.
Amesema
Philemon Foundation kwa kutambua kuwa wazee ni hazina, wameamu kuangalia ni
jinsi gani ya kutumia hazina hii ya wazee ili waweze kutumika katika jamii
kutoa ushauri, kutoa elimu pamoja na ujuzi mbalimbali.
Kwa
upande wao baadhi ya wazee walioshiriki maadhimisho hayo wamelalamikia kitendo
cha vijana kuwanyanyapaa wazee wastaafu wenye ujuzi pindi waitwapo kazini
kufanya kazi za mikataba ya muda mfupi na kuwaona kama hawafai kuwapo kazini.
Pamoja na
mambo mengine Taasisi ya Philemon Foundation imezindua Sinior Citizen Club,
ambayo itahusika kwa karibu na wazee katika masula mbalimbali yakiwamo ya
kubadilishana mawazo, kupeana fusa mbalimbali pamoja na kutoa elimu mbalimbali
zitakazowasaidia.
0 Maoni