Nimepokea uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa moyo wa
shukrani. Quran Tukufu inatufundisha kuwa Allah ndie mpangaji na ni bora kwetu.
ALHAMDULILLAH.
Ndugu zangu wanaTanga Mjini, nitumie fursa hii kuwashukuru
kwa kuniamini kuwa Mbunge wenu kwa kipindi cha miaka 5 (2020 - 2025) Nafurahi
kuona kuwa utumishi wangu kwenu umewagusa wengi na umeacha alama kubwa za
kimaendeleo katika Jimbo letu. Asanteni kwa ushirikiano mzuri mlionipatia ktk
kipindi chote cha Utumishi wangu.
Kwa dhati ya moyo wangu, ninawashukuru wajumbe wa Mkutano
Mkuu maalum wa CCM Wilaya ya Tanga kwa kunipa kura nyingi ktk mchakato wa kura
za maoni za kutafuta mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo letu Tanga Mjini kwa
kipindi cha 2025 - 2030. Mlinikopesha imani kubwa sana Nitaienzi na kuithamini
imani hii daima.
UAMUZI wa vikao vya Chama ni lazima UHESHIMIWE. Nampongeza
Ndugu Kassim Amar Mbaraka (Makubel) kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM
Tanga Mjini.
Ninawaomba wanakimji wenzangu hususani wanaCCM tumpokee na
tumpe ushirikiano ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa Rais Dkt Samia,
Mbunge Kassim Makubel na Madiwani katika kata zote 27 za Jimbo la Tanga Mjini.
Mwisho, ninawashukuru wote kwa salaam za heri, sala na dua
zenu kwangu. Nimeuona upendo wenu. Asanteni sana. Allah ni Mkarimu.
Ndugu yenu,
Ummy Mwalimu
#OdoUmmy
#OktobaTunatiki
0 Maoni