Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango amekabidhi tuzo kwa
Wizara ya Maliasili na Utalii kufuatia
utendaji mzuri wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), tuzo ambayo
imepokelewa na Naibu Waziri Mhe. Dunstan Kitandula kwa niaba ya Mhe. Pindi
Hazara Chana, Waziri wa Maliasili na Utalii.
Tuzo hiyo imetolewa kwenye ufunguzi rasmi wa Mkutano wa Majadiliano wa Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Serikali ulioandaliwa na Msajili wa Hazina katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha.




0 Maoni