Kwa mara ya kwanza wananchi wa Kata ya Mpemba na Mpande wananufaika na kufurahia matunda ya ujenzi wa barabara itakayochochea kasi ya ukuaji wa uchumi na Maisha yao kwa ujumla.
Mhandisi
Yusuph Shabani Meneja TARURA Wilaya ya Momba ndani ya Halmashauri ya Mji wa
Tunduma amesema wamejenga barabara ya Mpande - Katenjele inayounganisha Kata
hizo.
Amesema
barabara hiyo ina urefu wa Km. 8.24 na tayari imekamilika na imejengwa na
Mkandarasi HSS ENGINEERING kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.
"Huko
nyuma barabara hii haikuwepo na wananchi wa maeneo haya ambao kimsingi
wanajihusisha na shughuli za kilimo, walikuwa wanapata changamoto kubwa ya
usafirishaji wa mazao yao kuyatoa maeneo ya mashambani kuyapeleka sokoni.
"Lakini
sasa kama mlivyowasikia wenyewe wanatoa ushuhuda huo kwamba sasa barabara hii
itawasaidia kuhakikisha mazao yao ambayo wanavuna yanafika sokoni kwa wakati.”
"Walikuwa wakipita kinjia kidogo sana,
sasa tumeifungua na wanapita,” aliongeza.
Mhandisi
Yusuph amebainisha wana jumla ya Halmashauri mbili wanazozihudumia ambazo ni
Halmashauri ya Mji Tunduma na Halmashauri ya Wilaya Momba.
"Tunduma
tuna barabara zenye urefu wa Km. 230.5 na Momba Km. 649.21 jumla Km. 879.71
kama Taasisi tumekuwa na utaratibu wa kuhudumia barabara zetu kwa matengenezo
ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi, matenegenezo ya vipindi maalumu na
miradi ya Maendeleo.
"Kimsingi
sasa tunapokea bajeti kutoka maeneo mbalimbali kuna bajeti inayotokana na fedha
ya Mfuko wa barabara (Road Fund), mfuko wa Jimbo(Constituency Fund), na fedha
zinazotokana na tozo ya mafuta ambazo tumeanza kuzipokea toka mwaka wa fedha
2021/2022.
"Fedha
hizi zimetusaidia kufanya kazi kubwa sana hasa kufungua barabara nyingi na
kuzifanyia matengenezo barabara ambazo kimsingi huko nyuma zilifunguliwa lakini
zilikuwa na hali mbaya.
"Katika
Wilaya yetu ya Momba tuna kanda tatu yaani Mji wa Tunduma, Ukanda wa Juu
(Halmashauri ya Mji wa Momba) na Ukanda wa Chini eneo ambalo ndipo ilipo Makao
Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba .
Amesema eneo
hilo la ukanda wa chini ndio eneo lenye changamoto kubwa kutokana na jiografia
yake kuwa na mito mingi na mikubwa inayopeleke maji katika Ziwa Rukwa,"na
barabara zipo katika hali ambayo tumeendelea kupambana nazo kuhakikisha
zinapitika katika kipindi chote cha mwaka.
"Kupitia
fedha zetu za mfuko wa Jimbo katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba tumefungua
barabara karibu Km. 50 mpaka sasa barabara mpya kabisa ambazo hazikuwepo
tumeendelea kuzifungua," amesisitiza.
Ameongeza
katika Halmashauri ya Wilaya ya Momba tumekuwa na miradi mikubwa miwili ya
kimkakati. Kwanza mradi wa kupunguza mlima
mkali barabara ya Ikana –Makamba, ili kuhakikisha tunafungua mawasiliano
kati ya eneo la Ukanda wa juu na chini ..Eneo lile la mlimani lilikuwa
halipitiki magari yalikuwa hayawezi kufika kwa urahisi, hivyo wafanyabiashara
walishindwa kusafirisha mazao yao kutoka Ukanda wa Chini kuleta Ukanda wa juu.
"Tumepunguza
ule mlima kiasi ambacho magari sasa ya wafanyabiashara yataweza kutoka Ukanda
wa Chini ambao ni wa kilimo na kufika juu ambako ni Ukanda wa kibiashara”.
Ameongeza
"Mkandarasi Sasa yupo 'site' anaendelea na kazi ya kumwaga zege (Rigid Pavement) sehemu ya mlima
huo na kwa mipango tuliyojiwekea tutaendelea kufanya hivyo kwa awamu kadri
ambavyo tunaendelea kupata fedha.
"Pia kwa
kutumia fedha hizo za mfuko wa mafuta tuna mradi mwingine mkubwa wa Ujenzi wa
daraja la Msangano linalounganisha makao
makuu ya Wilaya na Mji wa Tunduma , kazi hii inaendelea na imefikia asilimia 50
ya utekelezaji."
"Eneo
lile ilikuwa changamoto kwa maana ya Mawasiliano kati ya Ukanda wa kibiashara
na Ukanda wa Chini, tukifungua litakuwa limeunganisha na kurahisisha shughuli
za kiuchumi kwa wakazi wa Tarafa za Msangano na Kamsamba .
“Tukimaliza
daraja lile Septemba mwaka huu na kuifungua barabara wakulima wanaolazimika
kusafirisha mazao yao watapita moja kwa moja na kuja eneo la kibiashara Mji wa
Tunduma”Amesisitiza
"Tunaendelea
kupambana kuhakikisha linapitika na kurahisisha shughuli za kibiashara kwa
wananchi wetu wa Wilaya ya Momba," amesema.
Kwa upande wa
Mji wa Tunduma mjini wameweza kupambana
kwa fedha za mafuta, Jimbo na maendeleo ambapo wameweza kujenga barabara za
lami yenye jumla ya urefu wa Km. 10.27. “Ili kuhakikisha tunapunguza Msongamano
wa magari katikati ya Mji, tumependekeza ujenzi wa barabara ya Mchepuko kupitia
Mradi wa TACTICS awamu ya tatu yenye urefu wa Km. 10.2 ambayo ikikamilika
itapunguza msongamano wa magari katikati ya mji kwa magari yote yanayoelekea
Sumbawanga hayatalazimika kupitia mjini.
"Tumeweka
taa 95 za barabarani na mpango uliopo sasa kupitia bajeti yetu fedha za mfuko
wa Jimbo 2025/2026, tumekusudia kuweka taa barabarani ili wafanyabiashara
wafanye kazi saa 24, hata hivyo taa zilizopo wanafurahia na maeneo ya mjini
wanaendelea kufanya biashara hata wakati wa usiku
zinawasaidia," amesema.




0 Maoni