Msajili wa
Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amewataka watumishi wa ofisi yake kuutumia mwezi
mtukufu wa Ramadhani kama nyenzo ya kufanyakazi kwa bidii na maarifa makubwa
kwa faida ya Taifa la Tanzania.
Bw. Mchechu
aliyasema hayo jana Jumatatu, Machi 24, 2025 wakati wa hafla ya iftar kwa
watumishi wa ofisi ya Msajili wa Hazina iliyoandaliwa na Msajili wa Hazina
mwenyewe.
“Mwezi huu
unatufundisha uvumilivu, kujitolea, na huruma kwa wengine, maadili ambayo pia
yana nafasi muhimu katika mazingira ya kazi,” alisema Bw. Mchechu wakati wa
hafla iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya KingJada, Morocco Square, Dar es
Salaam.
Aliongeza:
“Natumai kila mmoja wetu ataendelea kuyaishi haya mafunzo hata baada ya mwezi
huu kumalizika.”
Bw. Mchechu
alielezea kutambua na kuthamini mchango wa kila mtumishi katika mafanikio ya
OMH, na kusema kuwa ni matarajio yake kuwa roho ya mshikamano itaendelea hata
baada ya Ramadhani.
Alisema
leongo la kuwaleta pamoja watumishi ili wapate Iftari si tu ni kuvunja funga,
bali pia kuimarisha mshikamano wa watumishi kama familia moja ya Ofisi ya
Msajili wa Hazina.
“Ni furaha
kubwa kuwa pamoja nanyi katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa rehema,
msamaha na baraka nyingi,” alisema Bw. Mchechu.
Alitoa wito
kwa watumishi kuwaombea wenzao walioko mbali, jamii za Tanzania, na taifa kwa
ujumla, ili waendelee kuishi kwa amani, afya njema, na mafanikio.




0 Maoni