Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki
Mkutano wa Pamoja wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya
mtandao jana tarehe 24 Machi, 2025 Ikulu ndogo ya Mkanyageni, Chake Chake, mkoa
wa Kusini Pemba.
Mkutano huu
ni wa pili kufanyika baada ya ule wa kwanza uliofanyika tarehe 08 Februari,
2025 Ikulu, Jijini Dar es Salaam na ulihudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali
wafuatao:-
Rais William
Ruto wa Kenya, Dkt. Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, Rais Cyril Ramaphosa wa
Afrika Kusini, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais
Lazarus Chakwera wa Malawi, Rais Andry Rajoelina wa Madagascar, Rais Hakainde
Hichilema wa Zambia, Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania pamoja na Waziri Mkuu wa Somalia pamoja na Mawaziri kutoka Sudani
Kusini na Angola.



0 Maoni