Mbunge wa wa jimbo la Chalinze ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mh. Ridhiwani Kikwete amesema kuwa kumuombea Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni uzalendo kwa nchi.
Mh. Kikwete ametoa kauli hiyo wakati akiwahotubia wananchi
waliojitokeza kuomba dua ya kuiombea Nchi na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nyumbani kwake Msoga, Chalinze.
Akizungumza na umma wa Watanzania waliojitokeza kwenye dua hiyo, Mh. Kikwete amewashukuru kwa kujitokeza na kumuombea dua Mh. Rais. “ukimuombea Rais Samia, umeiombea Tanzania, kutokana na umuhimu wa nafasi yake na yeye akiwa ndiyo mshika maono ya nchi.”
Mh. Kikwete alitumia nafasi hiyo pia kuishukuru serikali ya
awamu ya 6 kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka hii ya
Rais Samia Suluhu Hassan ambapo Elimu, Afya, Miundombinu n.k na kutumia nafasi
hiyo pia kuwaomba wanachalinze waendelee kumuamini na kumchagua tena kwa kura
nyingi.
Wakizungumza baadhi ya masheikh waliohudhuria shughuli hii,
wamepokea maombi ya Mbunge wao kwa furaha na hivyo watatekeleza kwa ari kubwa.
Dua na Futari ni utaratibu ambao Mbunge wa jimbo la Chalinze amekuwa anafanya kila mwaka kipindi hiki cha Mfungo.
0 Maoni