WAZIRI MKUU,
Kassim Majaliwa leo Machi 24, 2025 ameshiriki futari na watoto wenye mahitaji
maalum wa shule ya msingi Buigiri iliyopo Chamwino Mkoani Dodoma inayomilikiwa
na kanisa la Anglikana Tanzania.
Akizungumza
na watoto hao Mheshimiwa Majaliwa amewaeleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
anatambua changamoto za watu wenye mahitaji maalum na mara zote anawezesha
utatuzi wake.
Kadhalika
Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwaasa watoto wenye mahitaji maalum
nchini kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo yao “Tumieni nafasi ya kuwa
hapa kusoma sana, wasikilizeni walimu wenu, wako kwa ajili yenu.”
Aidha,
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inaunga mkono taasisi za dini
kaunzisha maeneo ya kuwahudumia watanzania kwenye sekta mbalimbali za huduma za
kijamii. “Serikali pamoja na viongozi wa dini tunafanya kazi kwa pamoja.”
Kwa upande
wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu)
Patrobas Katambi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imefanikiwa kufufua
vyuo sita vya watu wenye ulemavu ambavyo vilikuwa vimefungwa kwa zaidi ya miaka
kumi.
Mheshimiwa
Katambi amesema Serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 3.2 kwa ajili ya
ukarabati wa vyuo hivyo “Pia Mheshimiwa Rais ametoa shilingi bilioni 3.4 kwa
ajili ya ujenzi wa vyuo vingine vipya vya watu wenye ulemavu na tumeanza ujenzi
kwenye mikoa ya Mwanza, Ruvuma na Kigoma.”





0 Maoni